Thursday, March 27, 2014

BASEL WALIMWA ADHABU NA FAINI KWA VURUGU ZA MASHABIKI.

KLABU ya Basel imethibitisha kuwa hawatarajii kukata rufani kupinga adhabu ya kufungiwa uwanja wao iliyotolewa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kufuatia vurugu za mashabiki zilizozuka katika mchezo dhidi ya Red Bull Salzburg. Kamati ya nidhamu ya UEFAilitangaza jana kuwa mabingwa hao wa soka wa Switzerland wanatakiwa kucheza mechi yao ya mkondo wa kwanza ya robo fainali ya Europa League dhidi ya Valencia bila mashabiki baada ya kukutwa na makosa mawili ya vurugu za mashabiki wake huko Austria. Mwamuzi Manuel Grafe alilazimika kusimamisha mchezo baada ya mashabiki wa Basel waliosafiri kwenda kutizama mechi hiyo kurusha mafataki katika Uwanja wa Red Bull Arena wakikasirishwa na kadi nyekundu aliyopewa Marek Suchy sambamba na bao la Jinatan Soriano. Basel ambao pia wametozwa faini ya euro milioni 107,000 pamoja na kucheza huku milango ikiwa imefungwa, wameamua kutokana rufani juu ya adhabu hiyo na kulaani vikali vitendo hivyo vilivyofanywa na mashabiki wao.

No comments:

Post a Comment