Monday, January 16, 2012

GHANA YAFURAHISHWA NA UJIO WA ESSIEN.


SHIRIKISHO la Soka nchini Ghana-GFA limesema limefurahishwa kwa hatua ya kiungo wake Michael Essien kurejea uwanjani baada ya kukaa nje kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua. Essien alikuwa nje ya uwanja karibu miezi sita na matokeo yake amekosa fainali zingine za Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza Januari 21 mwaka huu huko Gabon na Equatorial Guinea. Rais wa GFA Kwesi Nyantakyi amesema katika taarifa yake kuwa kurudi kwa mchezaji huyo ni jambo kubwa kwa kwa klabu yake ya Chelsea pamoja na nchi yake. Nyantakyi aliendelea kusema kuwa pamoja na kwamba mchezaji huyo atakosa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika lakini wanamuombea kupona huko kumpe changamoto mpya ili hapo baadae aweze kurejea kulitumikia taifa lake.

No comments:

Post a Comment