Monday, January 16, 2012

BARCA YAJIPANGA KUPINGA KADI YA INIESTA.

MENEJA wa Barcelona Pep Guardiola amefafanua kuwa klabu hiyo inajipanga kukata rufani ili kupinga hatua ya mchezaji wake Andres Iniesta kupewa kadi ya njano katika mchezo baina ya timu na Real Betis ambao walishinda kwa mabao 4-2 katika Uwanja wa Camp Nou. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alipewa kadi hiyo kwa kujiangusha katika eneo la hatari katika kipindi cha pili cha mchezo huo ingawa hata hivyo ilionekana dhahiri kabisa kwamba beki wa Betis Jefferson Montero alimkwatua. Guardiola akihojiwa baada ya mchezo huo amesema kuwa haikuwa penati kwakuwa mwamuzi hakuona tukio lile vizuri lakini wanatarajia kupinga Iniesta kupewa kadi ya njano. Guardiola pia alikisifia kikosi chake kwa moyo wa kujituma walioonyesha kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment