Monday, January 16, 2012

MTANDAOWA TWITTER WAMKATISHA MTU MMOJA KWA KUTOA UJUMBE WA KIBAGUZI.

POLISI nchini Uingereza wamemkamata mtu mmoja kufuatia kutuma ujumbe wa kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwalenga wachezaji wawili wa Rangers. Mtu huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anashikiliwa na polisi baada ya malalamiko kuwa beki wa Rangers Kyle Bartley na mchezaji mwezie wa timu hiyo Maurice Edu kutumiwa ujumbe huo wakibaguzi kwenye Twitter. Bartley ambaye yuko kwa mkopo kwa mabingwa hao wa nchini Scotland akitokea klabu ya Arsenal aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa amesikitishwa sana na kauli ya huyo mtu na anashangaa kwamba mpaka kipindi hiki bado watu wana mambo kama hayo ila anaamini pilisi watafanya kazi yao. Edu naye aliandika katika ukurasa wake kuwa imekuwa ni siku mbaya kwake kuona kwamba watu wanafikiria kuandika ujumbe wa kibaguzi katika mtandao huo badala ya kupinga vitu hivyo katika karne hii.

No comments:

Post a Comment