Tuesday, January 17, 2012

HATIMAYE RONALDINHO ASAFIRI NA FLAMENGO.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Flamengo ya Brazil Ronaldinho amesafiri na kikosi hicho Jumatatu kuelekea nchini Bolivia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini. Ronaldinho amesafiri na timu hiyo pmoja na vitisho alivyotoa vya kutosafiri na kikosi hicho endapo hatalipwa mshahara wake wa miezi mitano ambao hajalipwa na klabu hiyo. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona na AC Milan amekuwa sehemu ya wachezaji 16 wanaounda kikosi hicho waliosafiri kwa ya mchezo wa ugenini dhidi ya timu ya Real Potosi. Wakala wa Ronaldinho Roberto Assis ambaye pia ni kaka yake amesema wamefikia makubaliano na klabu hiyo pamoja na kampuni ambayo inalipa sehemu ya mshahara wa mchezo kuwa watalipa fedha hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha euri milioni mbili Jumatano.

No comments:

Post a Comment