Tuesday, January 17, 2012
WE'RE FINALLY READ-AFCONS CO HOSTS.
WENYEJI wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchi za Equatorial Guinea na Gabon wana ukakika licha ya wasiwasi uliokuwepo na baada ya uwekezaji mkubwa waliofanya katika viwanja, barabara na mahoteli sasa wako tayari kwa ajili michuano hiyo mikubwa barani Afrika. Wakati wanakubaliana kuandaa michuano hiyo nchi hizo mbili ambazo zina utajiri mkubwa wa mafuta katika ukanda wa Magharibi mwa Afrika wamepitia katika magumu mengi mpaka kufikia hatua hiyo ya mwishoni. Equatorial Guinea imejenga kiwanja kimoja kipya chenye uwezo wa kuchukua watu 15,000 uwanja ambao umejengwa katika jiji la Malabo wakati uwanja uliopo katika jiji la Bata ambao ndio utakuwa wa ufunguzi wa michuano hiyo Jumamosi una uwezo wa kumeza watu 38,000. Gharama za viwanja vyote viwili zinakadiriwa kufikia kiasi cha euro milioni 75 huku asilimia 85 ya barabara za nchi hiyo zikiwa zimefanyiwa marekebisho na zingine kujengwa upya huku mahoteli katika jiji la Malabo nazo zikiwa zimefanyiwa marekebisho na nyingine zikiwa ni mpya. Wakati Equatorial Guinea ikifanya hayo hali ilikuwa tofauti kwa Gabon ambao wao walichelewa ujenzi kwani tokea mwaka 2006 walipopewa dhamana ya kuandaa michuano hiyo mpaka 2009 hakuna chochote kilichofanyika kwa ajili ya maandalizi hayo. Ilikuwa ni wakati Rais wan chi hiyo Ali Bongo Ondimba alipoingia madarakani kazi rasmi za ujenzi zilipoanza huku kamati ya maandalizi ikiingiwa na utata mkubwa baada ya kubadilisha viongozi wake mara tatu. Mwezi Machi mwaka jana Shirikisho la Soka la Afrika-CAF lilikiri kuwa na wasiwasi kutokana na maandalizi yanavyokwenda taratibu na matokeo yake uwanja wa kihistoria wa Omar Bongo umeshindwa kutumika katika michuano hiyo kwakuwa bado uko katika ukarabati. Michezo ambayo ilitakiwa kufanyika jijini Libreville sasa itachezwa katika Uwanja wa Amitie Agonje ambao ulimalizika Novemba mwaka jana wakati ukarabati wa Uwanja wa Franceville ukiwa ndio kwanza umekamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment