Tuesday, January 17, 2012

PIRES AFURAHIA MAISHA YA INDIA.

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Robert Pires ameweka wazi msisimko wake kufuatia ufunguzi wa kihistoria wa Ligi Kuu nchini India. Nchi hiyo ambayo imejikita zaidi katika michuano ya kriketi, Pires pamoja na mastaa wengine ambao walipata kutamba Ulaya watakuwa jijini Kolkata ambapo klabu sita zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo. Akihojiwa mchezaji ambaye mkataba wake wa mwaka mmoja na Aston Villa umemalizika amesema kuwa hana kitu cha kufanya Ulaya hivyo haoni sababu ya kutojaribu kitu kipya ambacho hakijulikani na hajawahi kufika huko. Chama cha Soka cha nchi hiyo kwa kushirikiana na kampuni Celebrity Management Group-CMG kwa pamoja wamepania kuitangaza ligi hiyo kwa kuwaleta wacheza nyota kutoka Ulaya kuchezea ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment