Wednesday, January 18, 2012

"IBRAHIMOVIC KUZEEKEA MILAN". WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji wa kimatifa kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic amedai kuwa mteja wake huyo anataka kumalizia soka lake akiwa na klabu ya AC Milan. Wakala huyo aitwaye Mino Raiola alisisiza kuwa hakuna ukweli wowote kuwa mteja wake huyo hana furaha katika klabu hiyo na anawaza kuikacha mwishoni mwa msimu huu. Raiola amesema tatizo kubwa linalomsumbua mteja wake ni kupoteza mchezo baina yao dhidi ya watani wao wa jadi Inter Milan kwa bao 1-0 Jumapili katika Uwanja wa San Siro na si zaidi ya hapo. Raiola alikiri pia Ibrahimovic bado alikuwa akihitaji Carlos Tevez kujiunga na klabu hiyo ingawa suala hilo kwasasa linaonekana halitawezekana baada ya timu hiyo kusimamisha mazungumzo na mshambuliaji huyo wa Manchester City.

No comments:

Post a Comment