Wednesday, January 18, 2012

PRINCE BOATENG NJE WIKI NNE.

KIUNGO wa AC Milan Kevin-Prince Boateng atakuwa nje uwanja kwa muda wa wiki nne kufuatia majeraha ya misuli yanayomsumbua. Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Jumatatu kiungo huyo aliumia katika mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya mahasimu wao Inter Milan ambapo Milan walipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0. Taarifa hiyo ilieleza kuwa mchezaji huyo alipata tatizo la msuli wake wa mguu wa kushoto kukamaa na atafanyiwa tathmini tena siku saba zijazo. Tatizo la majeruhi limekuwa likiiandama klabu hiyo na kumkosa Boateng itakuwa pigo kubwa baada ya viungo wengine Gennaro Gattuso na Alberto Aquilani kuwa nje ya dimba katika kipindi hiki.

No comments:

Post a Comment