Monday, January 23, 2012

TAARIFA KUTOKA TFF LEO.

WABUNGE KUCHANGIA TWIGA STARS 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya kuwasilisha mchango wao kwa timu hiyo. Benchi la Ufundi la Twiga Stars kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kucheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya maonesho tu ambapo baada ya kumalizika ndipo Wabunge watakabidhi kile walichopanga kutoa kwa timu. Mechi hiyo itafanyika Alhamisi (Januari 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume uliopo Ofisi za TFF kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars na Namibia zitapambana Jumapili (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.



GHARAMA ZA UWANJA- TWIGA STARS VS NAMIBIA
TFF imeiandikia Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuomba iondoe gharama za kutumia Uwanja wa Taifa ambazo ni fixed kwenye mechi kati ya Twiga Stars na Namibia. Lengo la maombi hayo ni kusaidia kupunguza gharama za kuandaa mechi hiyo ambayo bajeti nzima ni sh . 74,660,000. Hiyo inajumuisha usafiri, posho kwa wachezaji, posho kwa benchi la ufundi, gharama za kambi, dawa na maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi kwa Twiga Stars. Maeneo mengine ni usafiri wa ndege, usafiri wa ndani (magari mawili), posho na hoteli kwa kamishna na waamuzi. Nyingine ni gharama za timu ya Namibia itakayokuwa na watu 25 ambazo ni usafiri wa ndani (magari matatu), hoteli (malazi na chakula) na maji ya kunywa wakati wa mazoezi na mechi. Gharama ambazo ni fixed kwa matumizi ya Uwanja wa Taifa ni pamoja na usafi na ulinzi, umeme, maandalizi ya sehemu ya kuchezea, malipo kwa kampuni ya Wachina na asilimia kumi ya mapato.

No comments:

Post a Comment