Monday, January 23, 2012

MAKAMU WA RAIS WA GHANA ATEMBELEA KAMBI YA KIKOSI HICHO.

MAKAMU wa Rais wa Ghana John Dramani amewaonya wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo kutobweteka na sifa wanazopewa wakati wanatakapoanza safari yao ya kutafuta taji la tano la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambalo hawajalichukua katika kipindi cha miaka 30. Kauli ya Dramani imekuja kufuatia kutembelea kambi ya ya kikosi hicho marufu kama Black Stars nchini Gabon ili kuwaongezea morali katika michuano hiyo. Dramani amesema kuwa anasikia taarifa kutoka sehemu mbalimbali kwamba timu zenye majina makubwa hazijashiriki michuano hiyo hivyo itakuwa rahisi kwa Ghana na timu zingine kunyakuwa taji hilo kwa urahisi. Lakini makamu huyo wa rais aliwakumbusha wachezaji hao kuwa hizo timu kubwa ambazo hazikushiriki zilitolewa na timu ambazo zinashiriki michuano hiyo hivyo sio timu za kubeza kwani na zimeonyesha kwamba zinaweza. Katika msafara wa Dramani aliongozana na Waziri wa Habari Baba Jamal, Mkurugenzi Mkuu katika ofisi yake Roger Ansogwine, Maofisa wa Baraza la Michezo pamoja na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment