Monday, January 23, 2012

MOURINHO AGOMA KUJIBU MASWALI.

MENEJA wa Real Madrid Jose Mourinho amekataa kujibu maswali kuhusu taarifa zilizovuja kwamba kuna mpasuko katika chumba cha kubadilishia nguo cha klabu hiyo na kusema hakukasirika pale mashabiki wa klabu hiyo walimpomzomea wakati wa mchezo dhidi ya Atletico Bilbao Jumapili ambapo walishinda mabao 4-1. Madrid imepitia katika kipindi kigumu siku za karibuni baada ya kupoteza mchezo katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mfalme ambapo walifungwa mabao 2-1 na mahasimu wao Barcelona. Katika mchezo huo Pepe alionekana kwa makusudi akimkanyaga mkono Messi huku mwenyewe akipinga na kudai kwamba ilikuwa bahati mbaya lakini magazeti ya Hispania yamekuwa yakimshambulia kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana. Gazeti mo ja kubwa la nchi hiyo la kila siku la Marca liliripoti Jumapili kuwa Mourinho na beki wake Sergio Ramos hawakuwa katika maelewano mazuri wakati wa mazoezi Ijumaa na kusema kuwa kuna ufa mkubwa kati ya Mourinho na baadhi ya wachezaji wa kimataifa wa Hispania waliopo katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment