Thursday, January 26, 2012

AFCON 2012: KOCHA WA GUINEA AFIWA NA BABA YAKE.

WAKATI akipoteza mchezo dhidi ya Mali kwa bao 1-0 wakati wa mchezo wa kundi D Jumanne kocha wa Guinea Michel Dussuyer alipata pigo lingine katika muda huohuo baada ya kufiwa na baba yake huko kwao Ufaransa. Mwishoni mwa mchezo huo uliokuwa na upinzani mkubwa kocha huyo alipigiwa simu kupewa taarifa kuwa baba yake aliyekuwa na umri wa miaka 82 amefariki dunia. Akihojiwa Dussuyer amesema ulikuwa ni usiku usiokuwa mzuri kwake baada kumpoteza baba yake halafu muda huohuo kupoteza mchezo pia. Tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka 2008 katika michuano kama hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa Ivory Coast Ulrich Stielike aliiacha timu hiyo katikati ya mashindano baada ya kufiwa na motto wake kiume huko kwao.

No comments:

Post a Comment