Thursday, January 26, 2012

AFCON 2012: MASTAA SENEGAL WAAGA MAPEMA MICHUANO HIYO.

TIMU ya taifa ya Senegal inakuwa timu ya kwanza kuondoshwa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kukubali kipigo kutoka kwa wenyeji wa michuano hiyo Equatorial Guinea cha mabao 2-1. Senegal ambao waliingia katika michuano hiyo ikiwa ni timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakuwa michuano hiyo ilijikuta katika wakati mgumu baada ya wenyeji kutangulia kufunga bao dakika ya 62 kupitia kwa Iban Randy. Baada ya bao hilo Senegal walikuja juu na kusawazisha katika dakika ya 89 ya mchezo huo kabla ya mshambuliaji wa Equatorial Guinea kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 90 na kupeleka kilio kwa timu hiyo. Kwa matokeo hayo wenyeji hao ambao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wao waliojazana uwanjani watakuwa wametinga hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment