Thursday, January 26, 2012

BALOTELLI AKUBALI ADHABU YA MECHI NNE.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia na Manchester City Mario Balotelli ameanza kuitumikia adhabu yake ya kufungiwa michezo minne baada ya kukubali adhabu hiyo iliyotolewa na Shrikisho la Soka la Uingereza-FA kwa kumpiga kwa makusudi kiungo wa Tottenham Hotspurs Scott Parker katika mchezo wao wa Jumapili iliyopita. Balotelli mwenye umri wa miaka 21 alikosa mchezo wa Jumatano ambao timu yake ilitolewa katika nusu fainali ya pili ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool na pia atakosa michezo mingine mitatu ya Ligi Kuu nchini humo. Katika tukio alilofanya mchezaji huyo katika mchezo huo mwamuzi Howard Webb aliyechezesha mchezo huo hakumpa kadi ingawa baadae amesema kuwa kama angeona tukio hilo basi anngetoa kadi nyekundu kwa mchezaji huyo.   Michezo mingine ya Ligi Kuu ambayo Balotelli atakosa ni pamoja na mchezo baina ya timu hiyo na Everton, Fulham na Aston Villa.

No comments:

Post a Comment