Saturday, January 21, 2012

BLATTER ADAI URUSI IKO MBALI KATIKA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA KULIKO BRAZIL.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA amesema nchi ya Urusi tayari imeshajiandaa na Kombe la Dunia litakalofanyika nchini 2018 kuliko Brazil ambao wao wataandaa michuano hiyo 2014. Akiongea na waandishi wa habari nchini humo Blatter amesema Urusi tayari wako mbali katika maandalizi hayo kuliko Brazil ambapo tunapata matatizo mengi kuliko hapa. Blatter aliendelea kusema mpaka mwezi uliopita nchi hiyo iliyopo Amerika Kusini bado ilikuwa na matatizo katika viwanja vyake vya ndege, barabara na usafiri wa umma lakini haiko hivyo kwa Urusi. Urusi walipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo mikubwa kwa mara ya kwanza wakati walipoishinda Uingereza pamoja na nchi mbilimbili zilizokuwa nazo zikigombea nafasi hiyo ambazo ni Hispania na Ureno pamoja na Ubelgiji na Uholanzi Desemba 2010 mwaka juzi.

No comments:

Post a Comment