Saturday, January 21, 2012

AFCON 2012: TUNISIA, MOROCCO WAHUDHURIA IBADA KATIKA MSIKITI MMOJA NCHINI GABON.

TIMU za taifa za Tunisia na Morocco Ijumaa zilihudhuria ibada kwa pamoja katika msikiti uliopo jijini Libreville kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo inatarajiwa kuanza leo. Timu hizo ambazo zinatarajiwa kucheza Jumatatu walikaribishwa na Imam wa msikiti huo huku akiwaombea kufanya vizuri katika mchezo wao uliopo mbele yao. Kabla ya kukutana katika mchezo wa Jumatatu timu hizo ambazo ni mahasimu zitaendelea kuonana mara kwa mara haswa ikizingatiwa kuwa wote wamewekwa katika hoteli moja ya Laico iliyoko katika mji mkuu wa Gabon. Akihojiwa Nahodha msaidizi wa Tunisia Aymen Mathlouthi amesema mchezo baina yao na Morocco ni muhimu kushinda kwani ndio utakaoleta dira kwa mechi zao zote watakazocheza katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment