Saturday, January 21, 2012
AFCON 2012: GHANA YATUA GABON.
TIMU ya taifa ya Ghana ambayo inapigiwa chapuo kunyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu imetua katika jiji la Libreville Ijumaa jioni tayari kwa michuano hiyo na kupelekwa katika kambi yake iliyopo katika mji wa Fanceville. Ghana inatarajiwa kuanza mchezo wake ufunguzi na timu ya Botswana katika kundi D Jumanne kabla ya kucheza na Mali pamoja na Guinea michezo ambayo itachezwa katika Uwanja wa Franceville. Kocha wa Ghana Goran Stevanovic alimaliza maandalizi yake nchini Afrika Kusini Jumatano ambapo alishuhudia kikosi chake kikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Platinum Stars ya nchini humo. Ghana imeshawahi kutwaa taji Mataifa ya Afrika mara nne lakini haijawahi kutwa taji hilo tena kwa kipindi cha miaka 30 sasa hivyo huu utakuwa ndio wakati muafaka haswa ikizingatiwa kuwa timu vigogo zote zimetolea mapema katika hatua ya kufuzu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment