Tuesday, January 24, 2012

RUFANI YA BIN HAMMAM YASIKILIZWA CAS.

RUFANI ya aliyekuwa mgombea wa zamani wa Urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Mohamed bin Hammam ya kulisimamisha Shirikisho la Soka barani Asia-AFC kutochagua rais mwingine imesikilizwa Jumatatu na na Mahakama ya juu ya Michezo-CAS. Bin Hammam mwenyewe hakuhudhuria mahakamani wakati shauri lake hilo likisikilizwa na CAS na wakili wake kutoka Marekani Eugene Gulland alikataa kuzungumza lolote kwa waandishi wa habari. Bin Hammam alikata rufani kuzuia AFC kuchagua rais mwingine wakati yeye akijaribu kubadilisha adhabu aliyopewa na FIFA ya kufungiwa kujishughulisha na shughuli zozote za michezo maisha kutokana na kashfa ya kununua viongozi wa soka wa Caribbean ili wampigie kura. Kwasasa Zhang Jilong kutoka China ndio anakaimu nafasi ya Bin Hammam katika AFC na pia ndiye aliyechukua nafasi ya mjumbe wa FIFA ambayo Bin Hammam alikuwa akiishilia toka mwaka 1996.

No comments:

Post a Comment