Tuesday, January 24, 2012

GYAN FITI KUIVAA BOTSWANA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana Asamoah Gyan leo anatarajiwa kukiongoza kikosi cha nchi hiyo katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua. Mshambuliaji huyo amekuwa katika hatihati ya kutocheza michuano hiyo kufuatia kuumia kifundo cha mguu lakini imethibitika kuwa Gyan yuko fiti na atacheza mchezo wao wa ufunguzi katika kundi D dhidi ya Botswana jijini Franceville. Uwanja wa Franceville watakaotumia Ghana pia utatumiwa na timu zingine za kundi hilo kutoka Magharibi mwa Afrika ambao ni mahasimu timu za Mali na Guinea ambazo kila moja zitahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Timu zote nne zilizopo katika kundi D ndizo zilikuwa za mwisho kuwasili katika michuano hiyo ambayo imeandaliwa kwa pamoja na Guinea ya Ikweta na Gabon.

No comments:

Post a Comment