Tuesday, January 24, 2012

BALOTELLI KIKAANGONI TENA.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City Mario Balotelli ameshtakiwa kwa vurugu alizofanya wakati wa mchezo baina ya timu yake na Tottenham Hotspurs uliofanyika Jumapili. Balotelli alionekana akimgonga kichwani kiungo wa Tottenham Scott Parker lakini mwamuzi wa mchezo huo Howard Webb hakuchukua hatua yoyote huku Muitaliano huyo akifunga bao la penati dakika za majeruhi na kuipa ushindi timu yake wa mabao 3-2. Balotelli ambaye kwa kosa hilo anaweza kufungiwa michezo minne amepewa mpaka Jumatano jioni awe amekata rufani kuhusiana na tukio hilo. Kama akiamua kukata rufani ataweza kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool Jumatano lakini asipokata rufani anaweza kupata adhabu kubwa zaidi ya hiyo.

No comments:

Post a Comment