Monday, January 30, 2012

MCLEISH ATAKA FA ICHUNGUZE TUKIO LA VAN PERSIE.

MENEJA wa Aston Villa Alex McLeish amelitaka Shirikisho la Soka nchini Uingereza-FA kuchunguza kwa makini tukio la mshambuliaji wa Arsenal Robin va Persie kumpiga kiwiko mchezaji wake Carlos Cuellar wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa Kombe la FA Jumapili. Kocha huyo anadai kuwa ni bahati kwa mchezaji kukosa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko beki huyo wa kimataifa kutoka Hispania wakati wakigombania mpira wa juu dakika ya 64 ambapo katika mchezo huo Arsenal ilishinda mabao 3-2. Mwamuzi aliyechezesha mchezo huo hakuchukua hatua yoyote kwenye tukio hilo na MacLeish anahitaji FA kuangalia upya tukio hilo katika mkanda wa video ili kuona kama mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anahitaji adhabu au la. Kabla ya tukio hilo Van Persie alikuwa ameshafunga mabao mawili kwa njia ya penati na kuisaidia timu yake kutoka nyuma kwa mabao mawili mpaka ushindi na kuiwezesha timu hiyo kuingia mzunguko wa tano wa kombe ambapo sasa itakutana na mshindi kati ya Sunderland au Middlesbrough.

No comments:

Post a Comment