Monday, January 30, 2012

KOCHA SENEGAL AGOMA KUBWAGA MANYANGA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Senegal Amara Traore amekataa kubwaga manyanga kuinoa timu hiyo pamoja na vipigo vitatu walivyopata katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ukiwemo mchezo wa mwisho wa kundi A dhidi ya Libya. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo kocha huyo amesema kuwa hataachia ngazi kuinoa klabu hiyo kwakuwa bado ana nia thabiti ya kuendelea kuifundisha. Senegal iliingia katika michuano hiyo ikiwa ni timu inayopewa nafasi ya kunyakuwa kombe hilo lakini ilijikuta ikipoteza michezo yote mitatu kwa kufungwa mabao 2-1 katika kila mchezo. Naye kocha wa Morocco Eric Gerets alionyesha nia ya kubakia kukinoa kikosi hicho pamoja na timu yake ambayo nayo ilikuwa ikipewa nafasi kutolea mapema katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment