Thursday, January 26, 2012

BOLTON YAMNYAKUA BEKI WA NY REDBULL.

KLABU ya Bolton Wanderers imetangaza kumyakuwa beki wa kimataifa wa Marekani Tim Ream anayechezea klabu ya New York Redbull kwa ada ambayo haikuwekwa wazi. Beki huyo wa kati mwenye miaka 24 ambaye alitumia muda wa wiki nzima kufanya mazoezi na klabu hiyo ametia saini mkataba utakaomwezesha kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu. Ream ametua klabuni hapo ikiwa ni wiki moja tu toka Bolton imuuze beki wake wa kati wa kimataifa wa Uingereza Gary Cahill kwenda timu ya Chelsea. Kocha wa Bolton Owen Coyle amesema ujio wa mchezaji huyo itakakuwa ni ahueni kubwa baada ya kumpoteza Cahill na ni mategemeo yake atazoea haraka mikikimikiki ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment