Wednesday, January 18, 2012

MARADONA APATA NAFUU.

MCHEZAJI nguli wa zamani wa Argentina Diego Maradona amewahakikishia mashabiki wake kuwa yuko katika hali nzuri baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa mawe katika figo. Maradona ambaye ni kocha wa Al Wasl ya Falme za Kiarabu-UAE alifanyiwa upasuaji Dubai baada ya kupata maumivu ya tumbo lakini aliruhusiwa kutoka hospitalini jumatatu. Muargentina huyo anatarajiwa kurejea katika benchi la ufundi wakati kikosi chake kitakapopambana na timu ya Al Sharjah Jumatatu ambapo baadae wiki hii atakiongoza kikosi hicho mazoezini. Timu ya Al Wasl kwasasa inashika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo wakiwa na alama 12 nyuma ya vinara wa ligi hiyo timu ya Al Ain huku wakiwa wamebakiwa na michezo 11 kabla msimu kumalizika.

No comments:

Post a Comment