Friday, January 27, 2012

AFCON 2012: GABON, TUNISIA UWANJANI LEO KUTAFUTA TIKETI ZA ROBO FAINALI.

WENYEJI Gabon na bingwa wa zamani wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Tunisia zinaweza kusonga mbele katika hatua robo fainali ya michuano hiyo kama watashinda michezo yao ya leo ya Kundi C jijini Libreville. Gabon ambao ni wenyeji michuano wakishirikiana na Equatorial Guinea itabidi ishinde mchezo wake dhidi ya Morocco ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Tunisia Jumatatu. Morocco kama wakikubali kipigo katika mchezo huo watakuwa wametolewa katika michuano hiyo na hivyo kuwa timu ya pili kigogo kuyaaga mashindano hayo baada ya Senegal. Tunisia ambao waliwahi kushinda michuano hiyo wakati walipoiandaa miaka nane iliyopita watakuwa kibarua kizito cha kuifunga Niger ambao nao walipoteza mchezo wa kwanza kwa wenyeji Gabon.

No comments:

Post a Comment