Friday, January 27, 2012

GYAN HATIHATI KUIVAA MALI.

MSHAMBULIAJI wa Ghana Asamoah Gyan jana alilazimika kusitisha mazoezi kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu yaliyokuwa yakimsumbua. Gyan ambaye kwasasa anacheza soka Uarabuni alikuwa katika hatihati ya kukosa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kutokana na kusumbuliwa na misuli maumivu aliyoyapata mwezi uliopita. Mchezaji huyo alianza vyema pamoja na wenzake wanaounda kikosi cha Ghana lakini kabla muda wa mazoezi kuisha alitoka nje na kukaa benchi huku akifunga kifundo chake cha mguu kwa barafu.
Baadae alichukuliwa na madaktari wa timu hiyo na kusindikizwa katika hoteli waliyofikia ambayo haiku mbali na uwanja huo wa mazoezi kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Naye nahodha wa timu hiyo John Mensah pia hakushiriki mazoezi na kikosi hicho kwa siku ya pili kutokana na maumivu ya misuli yaliyokuwa yakimsumbua lakini daktari wa timu hiyo amesema hayawezi kumuweka nje kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment