Friday, January 27, 2012

RIBERY FITI KUIVAA WOLFSBURG.

VINARA wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bayern Munich wamejipanga kumrejesha winga wake machachari Franck Ribery kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Wolfsburg pamoja na maumivu ya mgongo yanayomsumbua mchezaji huyo. Ribery alifanya mazoezi pamoja na wenzake jana pamoja na kulalamika kusumbuliwa na maumivu ya mgongo ambapo baadae daktari wa timu hiyo Hans-Wilhelm Mueller alimfanyia uchunguzi. Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa mchezaji huyo toka alipopewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Cologne kabla ya Christmas mwaka jana. Munich inajipanga kurejea katika kiwango chake baada ya kufungwa mabao 3-1 na Borussia Moenchengladbach Ijumaa iliyopita lakini pamoja na kipigo hicho bado wanaongoza ligi kwa tofauti ya magoli huku wakiwa wamefungana alama sawa na Schalke na Borussia Dortmund.

No comments:

Post a Comment