Wednesday, January 25, 2012

MENSAH NJE MECHI MBILI.

John Mensah
NAHODHA wa timu ya Ghana John Mensah hatakuwa sehemu ya kikosi hicho katika michezo miwili iliyobakia katika hatua za makundi kufuatia kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo baina ya timu yake na Botswana. Mensah alipewa kadi hiyo dakika ya 66 baada ya kumwangusha mshambuliaji wa Botswana Jerome Ramatlhakwane wakati akiwa katika harakati za kufunga bao. Kwa mujibu wa sheria za Shrikisho la Soka Afrika-CAF Mensah mwenye miaka 29 atafungiwa mechi mbili kutokana na kadi hiyo hivyo kumfanya akose michezo miwili muhimu inayofuatia katika hatua za makundi. Hiyo ni kadi nyekundu ya pili kwa mchezaji katika michuano hiyo huku nyingine akiwa alipewa kwa kufanya kosa kama hilo katika michuano ya mwaka 2008 dhidi ya Nigeria ambapo Ghana ilifanikiwa kushinda mabao 2-1 na kutinga hatua ya nusu fainali.

No comments:

Post a Comment