Wednesday, January 25, 2012

KOCHA WA IVORY COAST AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUSAHAU RAHA ZA ULAYA.

Francois Zahoui
KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast Francois Zahoui amewatahadharisha wachezaji wake kusahau mazingira ya Ulaya katika vilabu wanavyocheza na kukumbuka kuwa wapo mazingira magumu ya katika michuano Kombe la Mataifa ya Afrika. Kauli hiyo imekuja kufuatia timu hiyo ambayo inapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa michuano hiyo kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sudan katika mchezo wao wa kwanza. Akihojiwa na waandishi wa habari Zahoui amesema wakati unacheza Ulaya kunakuwa na waamuzi ambao wanajua jinsi ya kufanya kazi yao pamoja na viwanja bora kabisa lakini katika mazingira ya Afrika tunacheza kwenye joto huku waamuzi wakifanya lile wanaloweza. Ivory Coast itacheza na Burkina Faso katika mchezo wake unaofuatia wa kundi B kesho huku ikiwa na mategemeo ya kuonyesha cheche zake kutokana na wachezaji nyota wanaocheza vilabu vikubwa Ulaya.

No comments:

Post a Comment