Thursday, January 19, 2012

MOURINHO AKUBALI LAWAMA KUFUATIA KIPIGO KINGINE KUTOKA KWA BARCA.

KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekubali lawama kufuatia kufungwa kwa kikosi chake mabao 2-1 dhidi ya Barcelona katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Ligi uliofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu jana usiku. Bao la mapema lilifungwa na mshambuliaji wake Criastiano Ronaldo lilishindwa kutosheleza kuipa timu hiyo ushindi baada ya bao la kusawazisha la Carles Puyol na ushindi la Eric Abidal kutoka kifua mbele huku wakisubiri mchezo wa marudiano Jumatano ijayo katika Uwanja wa Camp Nou. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mourinho amesema kuwa anakubali lawama zote haswa kama timu yake imefungwa kwani timu ikishinda inakuwa ni furaha kwa kila mtu na ukifungwa unakuwa peke yako na ana fahamu hilo kwakuwa kuwa yuko katika mchezo wa soka kwa muda mrefu. Mourinho pia amesema beki wake Pepe anafaa kuadhibiwa kama akikutwa na makosa ya kumkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi katika mchezo huo kitendo ambacho mwamuzi hakuona.

No comments:

Post a Comment