Monday, January 30, 2012

AFCON 2012: WENYEJI GUINEA YA IKWETA YAMUONGEZA MKATABA KOCHA WAO.

Baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika wenyeji wa michuano hiyo Guinea ya Ikweta wameamua kumuongeza mkataba kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Gilson Paulo mkataba wa mwaka mmoja. Kocha huyo kutoka Brazil alichukua kibarua cha kuinoa timu hiyo ikiwa ni wiki chache tu kabla ya mashindano hayo baada ya ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo kujiuzulu wadhifa wake kwa kutokuelewana na uongozi wa soka nchini humo. Paulo mwenye miaka 62 alikuwa amepewa mkataba wa miezi miwili tu kuinoa timu hiyo lakini kutokana na kazi nzuri aliyofanya kuiwezesha timu hiyo kushinda michezo yake miwili ya kwanza na kuingia hatua ya robo fainali wameamua kumuongeza mkataba huo kama zawadi. Taarifa iliyotumwa katika mtandao wa serikali ya nchi hiyo ilithibitisha kweli suala la kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja kocha huyo ambaye atakuwa akilipwa kiasi cha dola 15,000 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment