Thursday, April 23, 2015

SAGNA ADAI HAJUTII KUJIUNGA NA CITY PAMOJA NA KUSUGUA BENCHI.

BEKI wa klabu ya Manchester City, Bacary Sagna amesisitiza hajutii kuhamia Etihad pamoja na kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza toka aondoke Arsenal. Sagna alijiunga na City kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Arsenal kumalika Juni mwaka jana lakini amefanikiwa kucheza katika mechi 16 pekee toka ajiunge na mabingwa hao wa Ligi Kuu. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Arsenal Wenger, amekuwa akinyimwa namba na Pablo Zabaleta lakini mwenyewe amesema angefanya uamuzi kama huo kama angeambiwa arudie. Sagna amesema amesikia kauli nyingi kutoka kea mashabiki wanaodai kuwa angebakia Arsenal lakini mwenyewe anadhani alifanya uamuzi sahihi kuondoka na atafanya hivyo kama akiambiwa arudie.

No comments:

Post a Comment