Thursday, April 23, 2015

SKRTEL ASISITIZA KUBAKIA LIVERPOOL.

BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel amesema hana mpango wao kuondoka katika timu hiyo wakati wakala wake akitangaza mteja wake huyo kukaribia kukamilisha mazungumzo ya mkataba mpya. Skrtel in mmoja kati ya wachezaji kadhaa wa Liverpool waliokuwa wakihusishwa na tetesi za kuondoka Anfield majira ya kiangazi. Klabu za Wolfsburg na Napoli zote zimeripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Zenit St Petersburg Januari mwaka 2008. Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Slovakia ambaye amebakisha miezi 14 katika mkataba wake wa sasa aliosaini mwaka 2012, amesema hana mpango wa kwenda popote. Wakala wa mchezaji huyo Karol Csonto amesisitiza kuwa ofa pekee iliyopo mezani kea ajili ya mchezaji huyo ni mkataba mpya ambao anatarajia kutia saini mapema iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment