KLABU ya Manchester City inakabiliwa na wakati mgumu katika mbio za usajili wa kiungo wa Wolfsburg Kevin De Bruyne, kufuatia Bayern Munich nao kutangaza kumfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. Mkurugenzi wa soka wa City, Txiti Begiristain ameshafanya mazungumzo na wawakilishi wa De Bruyne na amekuwa akimtazama mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea akicheza kwa wiki kadhaa. Lakini De Bruyne ambaye aliwahi kuichezea Chelsea michezo tisa baada ya kusajiliwa kwa paundi milioni saba akitokea Genk Januari mwaka 2012, ameweka wazi nia yake ya kubakia Ujerumani. Wolfsburg wenyewe tayari wameonyesha nia ya kumuongeza mkataba mpya ambao utambakisha hapo mpaka mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment