Thursday, April 23, 2015

JAPANA KUWA MWENYEJI WA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza Japan kuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kea kipindi cha miaka miwili ijayo. Baada ya kuandaa michuano hiyo mara ya mwisho mwaka 2012, Japana inatarajiwa kuwa mwenyeji tena mwaka 2015 na 2016, huku kwa mwaka huu ikitarajiwa kufanyika Desemba 10 mpaka 20. Katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa Japan imeonyesha weledi mkubwa katika kuandaa michuano ya FIFA, zikiwemo fainali sita za Klabu Bingwa ya Dunia ambazo zimekuwa na mafanikio. Naye rais wa Chama cha Soka cha Japan-JFA, Kuniya Daini amesema nafasi hiyo ni nyingine ya kipekee kea wachezaji na mashabiki kushuhudia michuano mikubwa ya soka ya vilabu. JFA inatarajia kutangaza miji itakayotumika kwa ajili ya michuano hiyo ya siku 10 baadae ambapo bingwa mtetezi in mabingwa wa Ulaya Real Madrid.

No comments:

Post a Comment