Thursday, April 23, 2015

FULANA YAMPONZA GUARDIOLA.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limemfungulia mashitaka meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kea kuvaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya mwandishi wa habari za michezo aliyeuawa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana. Mwanahabari huyo Jorge Lopez alifariki baada ya teksi aliyokuwa amepanda akielekea hotelini kwake kugongwa na gari linalodaiwa kuwa lilikuwa limeibwa katikati ya jiji la Sao Paulo nchini Brazil mwaka jana. Guardiola alikuwa amevaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya uchunguzi wa kifo cha mwandishi huyo wakati wa mkutano wake na wanahabari kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto juzi. UEFA imesema kwamba Guardiola amechukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu kitendo alichofanya hakihusiani na masuala ya michezo. Kanuni za shirikisho hilo zinapiga marufuku kea mtu yeyote kutumia matukio ya kimichezo kwa shughuli zisizohusiana na suala hilo.

No comments:

Post a Comment