Thursday, April 30, 2015

JUVENTUS YAKUBALI KUMUUZA POGBA KWENDA PSG KWA EURO MILIONI 80.

KLABU za Paris Saint-Germain-PSG na Juventus zimekubaliana ada ya euro milioni 80 kea ajili ya uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtandao wa Goal, zimedai kuwa ofa ya PSG imekubaliwa na Juventus kea ajili ya usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye amekuwa mchezaji muhimu toka aondoke Manchester United mwaka 2012. Lakini pamoja na mabingwa hao wa Ufaransa kuonekana kukaribia kumnasa nyota huyo bado hakuna uhakika kama mwenyewe atakuwa kurejea jijini Paris. Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alikutana na Pogba na wawakilishi wake huko Monte Carlo mapema wiki hii lakini hawakufikia makubaliano ya masuala binafsi ikiwemo mshahara atakaolipwa. Inaaminika kuwa Pogba yuko tayari kusubiria ili kuona ofa nyingine ambazo anaamini zitakuja katika kipindi cha majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment