Thursday, April 30, 2015

ASTON VILLA KUMUUZA BENTEKE KWA EURO MILIONI 42.

KLABU ya Aston Villa itahitaji kitita cha euro milioni 42 kwa ajili ya mshambuliaji wake Christian Benteke ambaye anawindwa na Liverpool katika majira ya kiangazi. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amekuwa akimhusudu mshambuliaji huyo huku akiwa amepania kuimarisha safu yake ya ushambuliaji pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa. Wakala wa Benteke alidai mapema wiki hii kuwa hakuna timu iliyojitokeza kumtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji lakini Villa wenyewe wameamua kujitayarisha kama litatokea lolote. Meneja wa Villa Tim Sherwood anatarajia kuitaka klabu hiyo kuzuia ofa yeyote itakayotolewa kea ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu hiyo msimu huu huku akiwasaidia kutinga fainali ya Kombe la FA. Klabu za Manchester United na Tottenham Hotspurs nazo pia zinahusishwa na tetesi za kumtaka Benteke lakini Liverpool ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumchukua nyota huyo.

No comments:

Post a Comment