Thursday, April 30, 2015

HATMA YA DROGBA ITAAMULIWA NA ABRAMOVIC - MOURINHO.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amebanisha kuwa hatma ya mshambuliaji wake Didier Drogba iko mikononi mwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovic. Drogba alijiunga tena na Chelsea katika majira ya kiangazi mwaka jana kea uhamisho huru akitokea Galatasaray baada ya kuitumikia klabu hiyo miaka nane mara ya kwanza. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37 amecheza mechi 27 msimu huu wakati Chelsea ikikaribia kunyakuwa taji lake la kwanza la Ligi Kuu katika kipindi cha miaka mitano lakini anatarajia kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. Inaripotiwa kuwa Mourinho sasa anataka kuleta washambuliaji wapya vijana Stamford Bridge huku Charlie Austin wa QPR na Paulo Dybala wa Inter Milan wakipewa nafasi ya kuziba pengo la Drogba. Hata hivyo, Mourinho amefafanua kuwa mustakabali wa Drogba utaamuliwa na Abramovic na kuongeza kuwa nyota huyo amekuwa sehemu ya historia ya klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment