Friday, April 24, 2015

CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA KUKWAANA NA BAYERN.

KLABU ya Barcelona imepangwa kucheza dhidi ya Bayern Munich katika ratiba ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa leo. Katika mechi nyingine ya nusu fainali itawakutanisha Juventus ya Italia dhidi ya mabingwa watetezi wa taji hilo Real Madrid. Mechi za mkondo wa kwanza za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Mei 5 na 6 mwaka huu huku zile za marudiano zikichezwa wiki moja baadae. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa meneja wa Bayern Pep Guardiola kukutana kwa mara ya kwanza na timu yake ya zamani ya Barcelona ambayo aliiwezesha kunyakuwa mataji 13 akiwa kocha kwa kipindi cha miaka minne. 
Kwa upande wa michuano ya Europa League, Sevilla wao watakwaana na Fiorentina wakati Napoli wakipepetana na Dnipro ya Ukraine. Fainali ya Ligi ya Mabingwa inatarajiwa kuchezwa Juni 6 katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin Ujerumani wakati ile ya Europa League itachezwa Mei 27 katika Uwanja wa Taifa jijini Warsaw, Poland.

No comments:

Post a Comment