Thursday, April 23, 2015

WANYAMA AKANUSHA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ARSENAL.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Southampton, Victor Wanyama amekanusha taarifa kuwa amefanya mazungumzo na klabu ya Arsenal kwa ajili ya uhamisho majira ya kiangazi. Vyombo vya habari nchini Uingereza jana viliripoti kuwa Wanyama amefanya mazungumzo na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger na kuwa ana nia ya kujiunga nao mwishoni mwa msimu. Nyota huyo wa kimataifa wa Kenya aliadika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akikanusha taarifa hizo akidai kuwa hajawahi kuzungumza na Wenger kuhusiana na suala lolote kama inavyodaiwa. Wanyama aliendelea kudai kuwa anawaheshimu sana mashabiki wa Southampton ambao wamekuwa wakimuunga mkono toka alipowasili akitokea Celtic na angependa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

No comments:

Post a Comment