Thursday, April 30, 2015

MAMA WA MCHEZAJI KINGA ARSENAL ATIMULIWA KWA VURUGU.

KLABU ya Arsenal imemfungia mama wa mmoja wa wachezaji wao nyota chipukizi Ainsley Maitland-Niles baada ya mama huyo kumpiga mmoja ya wasaidizi wa meneja Arsene Wenger, Dick Law na kutishia kumtoa mwane uwanjani wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 21. Polisi waliitwa katika uwanja wa mazoezi wa Arsenal mwezi uliopita na kumkamata mama huyo kwa tuhuma za kufanya vurugu ingawa hakuna hatua yeyote zaidi iliyochukuliwa. Maitland-Niles msimu huu amekuwa mchezaji wa pili mdogo kuiwakilisha Arsenal katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wakati alipochukua nafasi ya Aaron Ramsey katika mchezo dhidi ya Galatasaray Desemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 17 na siku 102. Siku nne baadae chipukizi huyo anayecheza nafasi ya kiungo alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu katika mchezo dhidi ya Newcastle United ambao Arsenal walishinda mabao 4-1 huku pia akicheza kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Hull City.

No comments:

Post a Comment