Thursday, April 30, 2015

TORRES ANG'ARA ATLETICO IKIPATA USHINDI MWEMBAMBA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Atletico Madrid, Fernando Torres anaamini ameisogeza timu hiyo karibu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga bao la ushindi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Villarreal jana. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool alitumia vyema makosa ya Eric Bailly na kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 74 akiwa ameingia akitokea benchi. Mabingwa hao wakiwa alama saba juu ya Valencia waliopo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi, Torres ana uhakika kuwa watafuzu tena kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa. Akihojiwa Torres amesema katika mchezo huo walikaa na mpira kea kipindi kirefu lakini walishindwa kutengeneza nafasi ingawa hata hivyo wanashukuru kea ushindi huo mwembamba waliopata. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa bao lake hilo lina maana kubwa kwani wamejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani.

No comments:

Post a Comment