Thursday, April 30, 2015

PAMOJA NA MAN UNITED KUCHOMOA, PSG YAZIDI KUMKOMALIA DI MARIA.

WINGA wa Manchester United, Angel Di Maria bado anawindwa na klabu ya Paris Saint-Germain-PSG ambao wamepania kumsajili majira ya kiangazi. United wao imesisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza winga huyo ambaye alivunja rekodi ya usajili wa paundi milioni 59.7 mwaka jana. Lakini hata hivyo, nyota huyo wa zamani wa Real Madrid amekuwa akisugua benchi katika mechi tano za United zilizopita huku akishindwa kung’aa katika timu hiyo kama ilivyotegemewa. PSG walijaribu kumsajili Di Maria majira ya kiangazi mwaka jana lakini mipango yao ilishindwa kutokana na kubanwa na sheria za matumizi ya fedha za Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA.

No comments:

Post a Comment