Thursday, April 23, 2015

JUVENTUS SIO WASINDIKIZAJI LIGI YA MABINGWA ULAYA - ALLEGRI.

MENEJA wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri amesisitiza kikosi chake hakijaingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ili kutimiza idadi ya timu. Juventus maarufu kama vibibi vya Turin ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuiondosha AS Monaco kwa jumla ya bao 1-0 baada ya kutoka nao sare ya bila kufungana katika mchezo wa jana na kulinda ushindi wao wa bao 1-0 waliopata nyumbani wiki iliyopita. Akihojiwa Allegri amesema hawataogopa timu yeyote watakayopangiwa nayo katika nusu fainali kwani wamepania kwenda mbali zaidi ya hapo walipo. Mbali na Juventus, mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid nao walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuwabamiza majirani zao Atletico Madrid kwa bao 1-0 ambalo liliwekwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez katika dakika ya 88. Ratiba ya nusu fainali inatarajiwa kupangwa kesho ambayo itazijumuisha pia timu za Barcelona na Bayern Munich ambazo nazo zilifuzu baada ya kushinda mechi zao za juzi.

No comments:

Post a Comment