Thursday, April 30, 2015

WOLFSBURG YATAMBA KUICHAPA DORTMUND DFB POKAL.

MENEJA wa klabu ya Wolfsburg Dieter Hecking amesema kikosi chake kitafanya kila iwezalo kuhakikisha wanaichapa Borussia Dortmund katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ujerumani baada ya kuichapa Arminia Bielefeld. Wolfsburg wanaoshika nafasi ya pili walitinga katika hatua hiyo jana baada ya kushinda mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya timu hiyo ya daraja la tatu kwa mabao 4-0. Heckin ana uhakika kikosi chake kiko tayari kukabiliana na Dortmund ambao waliwang’oa Bayern Munich kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika nusu fainali nyingine iliyochezwa juzi. Kocha huyo amesema kwasasa wako imara na kikosi kipo katika kiwango ambacho walikuwa wakikihitaji. Heckin aliendelea kudai kuwa hajali timu gani watakayokutana nayo katika fainali kwani anachojua yeye wana uwezo wa kupambana na yeyote.

No comments:

Post a Comment