MCHEZAJI nyota wa Manchester City, Pablo Zabaleta amesisitiza kuwa yeye pamoja na wenzake wanapaswa kubeba baadhi ya lawama kea matokeo mabaya ya timu hiyo badala ya kumuachia meneja Manuel Pellegrini kubeba lawama zote. City wanatarajia kukabidhi taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu kea Chelsea msimu huu, kutokana na vijana hao wa Jose Mourinho kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kea tofauti ya alama 10 huku zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya msimu kumalizika. Kuporomoka kea City kumezusha mjadala juu ya mustakabali wa Pellegrini huku meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp na meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti wakitajwa kuja kuziba nafasi yake. Hata hivyo Zabaleta amesisitiza kuwa Pellegrini hapaswi kutimuliwa kwa matokeo yaliyotokana na kiwango kisichoridhisha kutoka kea wachezaji wake. Zabaleta amesema Pellegrini anastahili heshima kutoka kea kila mtu kwani alikuja kuanza kuinoa timu hiyo msimu uliopita na kunyakuwa taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa baadhi ya wachezaji pia wanapaswa kubebeshwa lawama kutokana na kutokuwa katika kiwango chao kwa msimu wotehuu.
No comments:
Post a Comment