WATU nane wameuawa katika klabu ya mashabiki wa soka jijini Sao Paulo, Brazil. Katika taarifa yake polisi wanadai kuwa mashabiki wa klabu ya Corinthians walikuwa wakiandaa mabango yao kuelekea katika mechi wakati watu wenye silaha walipowavamia. Wavamizi hao waliwaamuru mashabiki saba kulala chini kabla ya kuwafyatulia risasi na mtu wa nane yeye alipigwa risasi wakati akijaribu kukimbia. Polisi wanadai kuwa kuuawa kwa mashabiki hao wa kundi la Pavilhao Nove kunahusishwa na mambo ya madawa ya kulevya. Taarifa hiyo ya polisi iliendelea kudai kuwa kundi hilo la mashabiki huenda likawa na mahusiano na makundi ya kihalifu na mauaji hayo yanaweza kuwa na kulipiza kisasi na sio masuala ya soka. Vurugu katika soka nchini Brazil zimekuwa zikikua siku hadi siku huku mashabiki wa timu kadhaa kubwa za miji mikubwa wakitumia umaarufu wa vilabu vyao kuendesha shughuli za kihalifu nje ya uwanja.
No comments:
Post a Comment