Monday, April 20, 2015

MODRIC AIPA AHUENI MADRID.

KLABU ya Real Madrid imepata taarifa za ahueni baada ya Luka Modric kudai kuwa anaweza kurejea uwanjani kabla ya mwisho wa msimu. Kiungo huyo aliumia goti lake la kushoto katika mchezo wa La Liga dhidi ya Malaga na Shirikisho la Soka la Croatia lilitangaza siku iliyofuata kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita. Kwa upande wa klabu yake ya Madrid wao waligoma kutoa muda haswa ambao Modric atachukua kupona na mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs sasa amefafanua ana matumaini ya kupona kabla ya kumaliza kwa msimu huu. Akihojiwa Modric ambaye amerejea mwezi uliopita baada ya kupona majeruhi ya msuli, amesema kuumia tena ni jambo linalomuumiza haswa katika kipindi muhimu katika msimu lakini ana matumaini ya kurejea uwanjani mapema zaidi kuliko inavyokadiriwa.

No comments:

Post a Comment